Wito umetolewa kwa Wananchi kuondoa dhana potofu na mitazamo hasi iliyopo kuhusu ulaji na ulishaji watoto katika jamii na badala yake amewataka kuzingatia ulishaji bora kwa kufuata kanuni za Lishe.
Hayo yameelezwa Oktoba 30, 2024 na Bi Perpetua Eliya mwakilishi wa Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu Wilaya ya Kilosa Dokta Selemani Kasugulu Wakati wa maadhimisho ya Siku ya Lishe Kitaifa yaliyofanyika katika Kata ya Msowero.
Bi Perpetua amesema kuwa lengo kuu la Maadhimisho hayo ni kutoa Elimu ya Lishe kwa jamii huku malengo Mahsusi yakiwa ni kuelimisha jamii kufuata mapendekezo ya mwongozo wa Kitaifa wa Chakula na ulaji ili kuboresha Afya zao,Kuhamasisha Jamii kuhusu matumizi ya vyakula vilivyoongezewa virutubishi ili kukidhi mahitaji ya mwili kilishe.
Aidha kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni za ulaji unaofaa yaani kula Mlo kamili ili kukidhi mahitaji yote ya kilishe ili kuwa na Afya bora ,kupambana dhidi ya uelewa Duni,dhana potofu na mitazamo hasi iliyopo katika Jamii kuhusu masuala ya Lishe kwa kutoa taarifa sahihi na za kitaalamu.
Pia Kuelimisha na kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi na kushughulisha mwili ili kupambana dhidi ya Utapiamlo wa Lishe ya kuzidi, hivyo kuepuka magonjwa yasiyoambukiza yenye uhusiano na lishe kama vile Kisukari,Magonjwa ya Moyo,Shinikizo la juu la damu, Saratani na Magonjwa ya Figo.
Maadhimisho hayo yameambatana na Kauli mbiu maalumu isemayo ”Mchongo ni Afya zingatia unachokula”
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa