Wananchi Wilayani Kilosa wametakiwa kushiriki kampeni ya chanjo ya kichaa cha mbwa ili kufanya maboresho katika udhibiti wa ugonjwa wa kichaa cha mbwa na kuepuka madhara yasiyo ya lazima kwa jamii na mifugo.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na watafiti kutoka chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Afya cha Muhimbili kwa kushirikiana na AFROHUN chini ya mwamvuli wa AFYA MOJA ambayo ni nadharia inayokutanisha kada muhimu katika kutafuta suluhisho la matatizo ya afya katika jamii.
Akizungumza mmoja wa watafiti hao Bw. Jahashi Saidi Nzalawale amesema kuwa lengo la utafiti huo ni kutengeneza kitita cha mafunzo ili kuboresha ushiriki wa jamii katika kampeni ya chanjo ya kichaa cha mbwa.
Pia Bw. Nzalawale ameeleza kuwa ugonjwa wa kichaa cha mbwa ni hatari kwa binadamu na unaweza kupelekea kupoteza Maisha, ili kuepusha madhara hayo ni lazima chanjo itolewe kwa kiwango cha asilimia 70% ya mbwa wafugwao eneo husika.
Naye mkuu wa Divishioni ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo amesema kuwa Elimu inapaswa kutolewa mashuleni ili kuwepo na uelewa na ufahamu juu ya dalili za ugonjwa wa kichaa cha mbwa na jinsi ya kuthibiti ugonjwa huo ambapo elimu hiyo itasadia kuleta matazamo chanya kwenya jamii.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Rudewa Mhe. Subiri Joseph Mwamalili ameongeza kuwa jamii inapaswa kudhibiti mbwa ambao hawana wenyewe wanaotembea na kuishi masokoni ili nao waweze kupatiwa chanjo na wasilete madhara kwa binadamu na kwa mbwa wengine pia kuwepo na sheria ndogondogo katika ngazi ya Kijiji ambazo zitaelekeza jinsi ya kudhibiti ugonjwa huo wa kichaa cha mbwa ambao una madhara makubwa katika jamii.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa