Kinara wa lishe ni mtu ambaye kazi ndani ya jamii kwa lengo la kubadilisha fikra na kuleta matokeo katika lishe pamoja na kufanya ushawishi katika mapambano dhidi ya utapiamlo kuanzia ngazi ya jamii, kitaifa, kikanda na kimataif lakini pia ana dhamira ya kubadilisha maisha ya watu, fikra na vitendo vya kuboresha hali ya lishe.
Hayo yamebainishwa na Mkufunzi wa Lishe Endelevu Harriet Mkaanga wakati wa mafunzo kwa wanawake vinara wa lishe yaliyofanyika wilayani kilosa na kusema kuwa kinara ni shujaa katika sekta mbalimbali, kama vile siasa na michezo, lakini daima yuko tayari kutoa muda na rasilimali ili kuleta tofauti kubwa katika maisha lakini pia hutoa huduma kwa kujitolea.
Mkaanga amesema mwanamke kinara wa lishe anapaswa kuwa kiongozi bora ambaye yuko tayari na ana shauku kuhusu kile kinachoweza kufanywa na anawashirikisha watu anaowaongoza, muwajibika kwa matendo yake, anaomba ushauri na kusikiliza mawazo ya wengine,Muadilifu, anajiheshimu na kuheshimu wengineo, anapatikana mda wote na anategemewa lakini pia ni mwenye maarifa na mwelewa .
Akibainisha majukumu ya mwanamke kinara amesema anao wajibu wa kusaidia kuboresha au kupanua mipango na afua za lishe, ndani na nje ya maeneo yake, kukuza uzingatiaji ya lishe katika sekta mtambuka kama vile kilimo, mifugo, hifadhi ya jamii, kuhamasisha jamii kutekeleza majukumu katika kukuza agenda ya lishe. kuleta watu pamoja ili wawe na lengo moja, na uwezo wa kuendesha ajenda ya lishe kwa ajili ya mabadiliko, kujihusisha katika utetezi wa jamii, harambee za kuchangisha fedha na uhamasishaji wa rasilimali ili kuboresha lishe na kuwa na tabia chanya za lishe ili kuwa mfano wa kuigwa katika mabadiliko ya tabia ya jamii.
Akizungumzia upande wa umuhimu wa lishe bora Afisa Lishe Wilaya Zaina Kibona amesema lishe bora inasaidia kupunguza kiwango cha vifo vya watoto wachanga ambao kwa kiasi kikubwa huhusishwa na utapiamlo, Lishe bora inapunguza viwango vya kudumaa ambayo kwa kawaida huathiri pato la Taifa, kwa wanawake ambao wako kwenye umri wa kuzaa lishe bora inasaidia kupunguza upungufu wa damu na vifo vitokanavyo na uzazi, inasaidia uzalishaji, uchumi kukua, kupunguza umaskini kwa kuboresha uwezo wa mwili kufanya kazi, utambuzi, ufaulu shuleni, na kuimarisha afya lakini pia husaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza mf. kisukari, shinikizo la damu n.k.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa