Katika kuiadhimisha siku ya wazee Duniani wito umetolewa kwa wanawake wazee kujiunga na vikundi vya wanawake kwa lengo la kufanikisha azma ya kupata mikopo ya 10% inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya wanawake , vijana na wenye ulemavu.
Akitoa wito huo katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Oktoba Mosi mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh. Alhaj Majid Mwanga amesema mikopo hiyo kwa kundi la wanawake haina mipaka ya umri hivyo ni vema akatumia fursa hiyo wakati Serikali ikendelea kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuwasaidia wazee kwa ujumla wao.
Aidha katika maadhimisho hayo ya siku ya wazee duniani yenye kauli mbiu ya Matumizi Sahihiya Kidigitali Kwa Ustawi wa Rika Zote ametoa onyo kwa watendaji wote wa vijiji wanaodai fedha kwa watu wanaokwenda kuchukua vitambulisho vyao vya Uraia katika ofisi za vijiji kuwa vitambulisho hivyo vinapaswa kutolewa bila gharaama yoyoyote huku akisisitiza kundi la wazee na wananchi wote kufika katika ofisi za vijiji ili kuchukua vitambulisho vyao vya uraia.
Akisoma Risala hiyo ya Wazee Bi Leah Mzuamtemi Nzali amebainisha changamoto zinazowakabili wazee hao ikiwemo Umasikini, kutokuwepo katika mfumo wa Hifadhi ya jamii hususani wazee waliostaafu katika ajira zisizo rasmi kama vile kilimo, ufugaji, uvuvi, magonjwa, kutokushirikishwa katika mipango ya maendeleo, kutokuwepo kwa mfuko wa wazee, kutopatikana kwa vitambulisho vya taifa(NIDA) kwa wazee, huduma mbovu na kutozwa gharama za matibabu kwa wazee.
Katika kufanikisha maadhimisho ya siku ya wazee duniani Mganga Mkuu Mkoa wa Morogoro Dokta Kusirye Urio akiwa ameambatana na timu ya madaktari wametoa itatoa huduma mbalimbali kwa watu wote waliofika katika maadhimisho hayo ikiwemo utoaji wa chanjo ya UVICO19 kwa hiyari, upimaji wa maradhi mbalimbali bure pamoja na zoezi la uchangiaji damu salama.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa