Wasimamizi wa Elimu wilayani Kilosa wametakiwa kuipa kipaumbele Elimu ya watu wazima ili kuleta uwiano sawa wa kielimu kwenye jamii.
Wito huo umetolewa Septemba 25, 2024 na Afisa Tawala Wilaya ya Kilosa Salome Mkinga wakati wa hotuba yake katika maadhimisho ya kilele cha Juma la Elimu ya Watu Wazima yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Lamulilo iliyopo Kata ya Magomeni.
Bi.Salome Mkinga Amewataka Walimu Wakuu na Maafisa Elimu Kata kusimamia elimu ya watu wazima ili kuendana na sera ya Serikali ya Elimu ya watu wazima.
Aidha amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua mchango wa Elimua ya watu wazima ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa za elimu ya sekondari na msingi kwa wale waliozikosa elimu hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Bi. Zakia Fandey amesema kuwa Elimu ya watu wazima ina umuhimu kwani inawagusa watu wote kwenye jamii.
Akisoma Risala kwa Mgeni rasimi, Afisa Elimu anayeshughulikia elimu ya watu wazima Richard Mpumilwa amesema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ina jumla ya vituo 26 vilivyosajiliwa kutoa elimu ya watu wazima.
Miongoni mwa wadau waliohudhuria maadhimisho haya ni Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia na Watoto na Hemedi Rajabu Chabu ambaye ni Afisa wa Jeshi la Polisi Kutoka Dawati la Jinsia Wilaya ya kilosa ameitaka+ jamii kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia ili waweze kutimiza haki yao ya elimu.
Maadhimisho haya yameyakutanisha makundi mbalimbali huku shughuli mbalimali zikifanyika ikiwemo maonesho ya zana na mbinu za ufundishaji wa Elimu ya watu wazima huku yakiwa yamebebwa na kaulimbiu isemayo:
Ujumuishi katika Elimu bila Ukomo kwa Ujuzi, Ustahimilivu, Amani na Maendeleo”
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa