Wasimamizi wa Mikopo ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ngazi ya Halmashauri wamepatiwa mafunzo kwa lengo la kuwawezesha wasimamizi hao kupata ujuzi, kuboresha utendaji kazi, kuongeza tija, ufanisi na kuimarisha usimamizi wa mikopo.
Mafunzo hayo yametolewa 8 Oktoba, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ambapo muwezeshaji wa Mafunzo hayo Bi. Neema Solomon amesema mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea uwezo wasimamizi hao na kupata uelewa juu ya usimamizi wa mikopo kwa vikundi hivyo.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii Alto Mbikiye amesema Katika kuleta ufanisi katika uratibu na usimamizi wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, kutakuwa na kamati ya uratibu wa mikopo ngazi ya mkoa, kamati za huduma za mikopo ya halmashauri na kata, pia kutakuwa na kamati ya wilaya ya uhakiki wa mikopo hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa