Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wametakiwa kutambua kuwa Tume ya Uchaguzi inategemea kupitia wao uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu utakuwa wa amani usio na malalamiko huku wakitakiwa kuhakikisha taratibu, sheria na kanuni zote zinafuatwa ili kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza kutoka kwa wapiga kura.
.
Rai hiyo imetolewa Agosti 7 mwaka huu na Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo la Kilosa na Mikumi Asajile Lucas Mwambambale ambapo amewataka washiriki hao kutambua kuwa wana jukumu kubwa na nyeti hivyowanapaswa kuzingatia wajibu na majukumu yao wanayoelekezwa ili kufanikisha zoezi zima la uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani
Aidha Mwambambale amewataka kutofanya kazi hiyo kwa mazaoea lakini pia kuhakikisha wanazingatia matakwa ya Katiba, sheria na kanuni zinazosimamia zoezi la uchaguzi na kwamba zoezi la uchaguzi kwa mwaka 2020 ni zoezi jipya na wala halifanani na zoezi la mwaka 2015.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa jimbo la Kilosa na Mikumi kuanzia tarehe 07/08/2020 hadi tarehe 09/08/2020.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa