Wito umetolewa kwa wataalam na wadau wa afya kutosita kushirikiana na Serikali katika kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watu wote ili kuwaepusha na madhira mbalimbali ambayo yanaweza kujitokeza ikiwemo vifo vya kinamama vinavyotokana na uzazi na watoto wachanga chini ya miaka mitano.
Akitoa wito huo Agosti 20 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi wakati akifungua kikao chenye lengo la kujadili vifo vya kinamama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga kinachoshirikisha wataalam wa afya toka wilaya zote za mkoa wa Morogoro pamoja na wadau wa afya ambapo ametaka wataalam hao kushirikiana na Serikali licha ya kutumia utaalam lakini pia kutumia mbinu mbalimbali zitakazosababisha watu wote kuzingatia kanuni zote za msingi za kiafaya ili kuepuka vifo vinavyoweza kuepukika.
Mgoyi amesema ipo haja ya kutumika kwa mbinu mbalimbali ikiwemo matumizi ya sheria ndogo ndogo ambazo zitapaswa kufuatwa kwani jambo la kupoteza maisha linagusa familia na taifa kwa ujumla na kwamba anategemea kupitia kikao hicho watatoka na mbinu mpya za kupunguza ama kuondoa kabisa vifo vitokanavyo na uzazi.
Akibainisha sababu za vifo ikiwemo kutokwa na damu nyingi kabla,wakati na baada ya kujifungua, kifafa cha mimba, kuharibika kwa mimba na uchungu pingamizi anategemea kuwepo kwa mbinu mbalimbali na mikakati ya kupunguza vifo hivyo ikiwemo kushirikisha ngazi zote za Serikali upande wa kutoa elimu na kwamba Serikali inatambua changamoto zilizoko katika sekta ya afya ikiwemo uhaba wa wataalam wa afya ambapo Serikali inafanya juhudi za kuajiri wataala wa afya.
Akihitibisha hotuba yake Mkuu wa Wilaya huyo amesema vifo vya kinamama na watoto vinaumiza kila mtu ambapo ametaka wataalam wa afya kujitafakari upya katika utendaji wao na kuzitazama huduma wanazotoa kwa mapana jambo litakalosaidia kupunguza idadi ya vifo ambavyo vimekuwa vikijitokeza pamoja na malalamiko huku akitaka wataalam hao kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya afya kwa maendeleo ya Mkoa wa Morogoro.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa