Wataalamu wa Kilimo ngazi ya kata Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wamepatiwa mafunzo ya kukusanya taarifa za vijana wanaojishughulisha na kilimo mifugo na uvivi kwa kutumia mfumo unaoitwa KOBO.
Mafunzo hayo yametolewa 20 Novemba 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Taasisi ya SUGECO Kupitia Mradi wa YEFFA ambapo lengo likiwa ni kuimarisha ushirikishwaji na uwezeshwaji wa Vijana katika kuzalisha ajira kwenye Sekta ya Kilimo.
Akizungumza juu ya Mradi huo Afisa Kilimo kutoka SUGECO Bi Jackline Jonathan amesema kuwa kuna Washirika mbalimbali ambao watashiriki kwenye utekelezaji hivyo amewataka Wataalamu hao kuwa makini na
kuchukua taarifa sahihi kwa vijana na kuepuka kufanya udanganyifu kwani kwa kufanya hivyo hawataweza kufikia malengo ya Mradi huo.
Naye Mkuu wa Seksheni ya kilimo Wilaya ya Kilosa Bi. Elina Danstan amesema kuwa Mafunzo hayo yatasaidia kupata kanzi data ya vijana itakayowasaidia wadau kuwafikia kwa urahisi Vijana hususan wanaofanya Kilimo wanaojishughulisha na Kilimo.
Amewataka vijana watakapofikiwa wasisite kutoa taarifa zao ili waweze kupata fursa mbalimbali zitakazojitokeza kwani Wilaya ya Kilosa imebahatika kupata wadau mbalimbali wa kilimo na biashara zinazohusiana na Kilimo.
Kwa upande wake Afisa Kilimo Kata ya Kisanga Bwana Efraimu Tulimbange Chisunga amesema kuwa kupitia mafunzo waliyoyapata watakuwa na uwezo kuwatambua vijana wanaojishughulisha na shughuli za kilimo wanazofanya
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa