Zaidi ya Shilingi milioni sitini na laki saba (60,700,000) zimetumika kununulia Pikipiki kwa Watendaji wa Kata 20 za Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato,usimamizi wa Miradi ya maendeleo,kuongeza uwajibikaji kwa kuzifikia jamii na kutatua migogoro ya Wakulima na Wafugaji kwa wakati.
Akizungumza katika zoezi la kuwakabidhi Pikipiki hizo Watendaji wa Kata 20,Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amesema hataki kusikia visingizio kwa Mtendaji kushindwa kufika katika Miradi na kusimamia shughuli za maendelea pamoja na kusaidia jamii katika kukabiliana na changamoto ya migogoro.
Amewataka Watendaji kufikia lengo la kupunguza kwa asilimia 90 migogoro ya Wakulima na Wafugaji ifikapo mwaka 2024,kwa upande mwingine amewataka kuzitunza vyema Pikipiki hizo ili ziweze kudumu kwa muda Mrefu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa,amesema kutokana na umbali wa vitongoji,vijiji na kata za Halmashauri hiyo, Uongozi ulitenga fedha shilingi milioni 60,700,000/= kwaajili ya kununua Pikipiki hizo kwa lengo la kuboresha utendaji kazi,kurahisisha shughuli za usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.
Akizungumza kwa Niaba ya Watendaji wenzake mara baada ya kukabidhiwa Pikipiki hizo ,Mtendaji wa Kata ya Mbigiri Niza Mgombele amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kuwapatia usafiri huo kwani utarahisisha utendaji kazi na kuleta tija.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa