Watendaji wa kata wametakiwa kuwajibika kila mmoja kwa nafasi yake badala ya kusubiri kufanya kazi na majukumu yao kwa kusukumwa kwani kila mtumishi wa umma anao wajibu wa kufanya majukumu yake bila kukumbushwa kwani suala la uwajibikaji ni la kila mtumishi wa umma.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Kisena Mabuba ambapo ametaka watendaji hao kuwajibika inavyostahiki huku akitaka kila mmoja kutimiza wajibu wake jambo litakalosaidia kupunguza manung’uniko kwa kutotimiza wajibu.
Kisena amesema kuwa kumekuwa na hulka kwa baadhi ya watendaji kutotimiza majukumu yao hususani katika utoaji wa taarifa na kuzibandika katika ofisi zao ili wananchi waweze kupata taarifa kwa wakati stahiki ambapo ametoa onyo kwa watendaji wasiowajibika hususani katika mazoezi mbalimbali ya kitaifa na kiwilaya yanayoendelea na na yanayotarajiwa kufanyika ikiwemo kutoa elimu na hamasa juu ya utoaji chanjo ya polio kampeni ambayo itazinduliwa kitaifa Aprili 28, 2022 lakini pia amewataka kusimamia uanzishwaji wa klabu za lishe mashuleni.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya Shaban Mdoe akisisitiza watendaji hao kutosubiri kukumbushwa kwani suala la afya ni jambo nyeti kwa maslahi mapana ya wananchi kwani huwezi kuwa na viongozi bora ama kuongoza wananchi ambao hawana afya bora hivyo ni vyema suala la lishe likazingatiwa ili wananchi wapate elimu lakini pia kuwa na afya bora.
Nao viongozi wa dini wametaka suala la afya za wananchi kuzingatiwa kwa umuhimu wake ili kuwa na jamii yenye siha njema ambapo wametaka mazoezi mbalimbali ya kitaifa yanayowekwa na viongozi yapewe umuhimu wake ikiwemo upataji wa chanjo ya Uviko-19, ushiriki wa zoezi la anwani za makazi, upataji chanjo ya polio kwa watoto chini ya miaka mitano itakayozinduliwa rasmi kitaifa tarehe 28/04/2022 na kufanyika kuanzia tarehe 28/04/2022 hadi tarehe 01/05/2022 na zoezi tarajiwa la sensa ya watu na makazi linalotegewa kufanyika mwezi Agosti 2022..
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa