Watendaji wa Kata Wilayani Kilosa wamepitia sheria ndogo ya kuzuia na kudhibiti Sumu Kuvu ili waweze kuzifahamu na kuzisimamia ipasavyo katika maeneo yao.
Akizungumza katika kikao hicho kilichoandaliwa na Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na TAMISEMI chini Mradi wa kudhibiti sumukuvu (TANIPAC) kilichofanyika Julai 11, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Afisa Kilimo Mkuu kutoka Wizara ya Kilimo Dodoma, Bi. Margaret Natai amesema kuwa mradi huo wa kupambana na Sumu kuvu umekuja na mikakati mbalimbali kama vile kujenga miundombinu ya hifadhi hasa maghala ya kuifadhia mazao, maabara ya kufanya uchunguzi, Chuo kitakachotoa mafunzo ya kudhibiti sumu kuvu pamoja na sheria ndogondogo zitakazoweka msisitizo kwenye kudhibiti sumu kuvu.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mhe. Wilfred Sumari amewashukuru viongozi wa mradi huo na kusema kuwa kupitia mradi huo Halmashauri imeweza kujifunza mambo mbalimbali kuanzia hatua ya mwanzo ya uandaaji wa shamba mpaka hatua ya mwisho uhifadhi wa mazao pamoja na sheria ndogo ndogo ya kuzuia sumu kuvu ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu.
Mhe. Sumari amewata watendaji kutekeleza na kusimamia vyema sheria hizo katika kata zao kuanzia ngazi ya chini ya kuzuia, kupambana na kudhibiti sumu kuvu.
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambaye ni pia ni Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Ndg. Betuely Ruhega amewata watendaji hao wa kata kutoa elimu na ushirikiano kwa wananchi ili waweze kupata ufahamu juu ya sheria hizo na kwamba itarahisisha katika utekelezaji wa kusimamia vyema sheria hizo .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa