Wito umetolewa kwa watendaji kata wilayani Kilosa kujitambua kuwa wao ni wawakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya na kwamba wanapaswa kusimamia kikamilifu shughuli zote za kata ikiwemo usimamizi wa ukusanyaji wa mapato unaofanywa na mawakala kwa njia ya mashine za POS.
Wito huo umetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ambaye pia ni diwani wa Kata ya Kisanga Mhe Hassan Kambenga wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupokea taarifa kwa robo ya pili kwa 2017/2018 katika ukumbi wa Kilosa Club wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Kambenga amesema kuwa watendaji wa kata wanawajibika na ni haki yao kufuatilia mwenendo mzima wa ukusanyaji mapato toka kwa mawakala kwani wao ndio wanaowajibika kutoa taarifa za maendeleo ya kata na kwamba mawakala hao wanapaswa kuwaheshimu na kuheshimu muundo wa utendaji kazi wa serikali.
’’Haiwezekana mawakala kuwavunjia heshima watendaji kwani ni maafisa wa serikali hivyo amewaonya vikali mawakala ambao wameonyesha utovu wa nidhamu kwa watendaji kwa kutoa kauli zisizo faa pindi watendaji hao wanapohoji kuhusu makusanyo na ameonya tabia hiyo iachwe mara moja na atakayebainika kuzuia taarifa za ukusanyaji wa mapato hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kutopatiwa tena mkataba wa kuendelea kufanya kazi ya ukusanyaji wa mapato’’. Kambenga amesisitiza......
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa