Waandikishaji wasaidizi ngazi yaJimbo wametakiwa kufuata kanuni na miongozo iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wakati wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linalotarajia kuanza tarehe 01 hadi 07, Machi, 2025.
Rai hiyo imetolewa na Afisa Mwandikishaji Jimbo Kilosa na Mikumi Betuely Ruhega wakati akihutubia katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandikishaji hao yaliyofanyika 22 Februari, 2025 katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Ilonga.
Waandikishaji hao wametakiwa kuhakikisha wapiga kura wote wapya wenye sifa za kuandikishwa, waandikishwe ili kupata haki yao ya msingi ya kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba, 2025.
Akiwaapisha waandikishaji hao, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Kilosa Agness Ringo amewataka kuepuka kufanya makosa yanayoweza kuathiri zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kutunza siri.
Uboreshaji huo unatarajia kuanza tarehe 01 hadi 07 Machi 2025 katika majimbo yote mawili yenye jumla ya vituo 421 vya uandikishaji.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa