Shirika lisilo la kiserikali linalowasaidia watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu ili kuondokana na umaskini (CAMFED) limewafadhili watoto hao kupata uelewa wa kozi mbalimbali zinazotolewa katika vyuo vya ufundi ili waweze kupata hamasa ya kujifunza stadi mbalimbali zinazotolewa katika vyuo hivyo.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Kamati ya CAMFED Wilaya ya Kilosa Claud Masambati wakati wa kutembelea vyuo hivyo Machi 13 mwaka huu ambapo amesema CAMFED imeamua kuwapatia watoto wa kike hamasa ya kujifunza zaidi katika vyuo vya wananchi lakini pia waweze kujua fani mbalimbali kama watoto wa kike kwani katika vyuo hivyo zipo fani ambazo wanaweza kujifunza na kuinua kipato badala ya kukaa majumbani na kushindwa kujikwamua kiuchumi ili kuepuka kuwa tegemezi.
Masambati amesema watoto hao wanaofadhiliwa na CAMFED ni wale ambao wako katika mazingira magumu ambao wanahitaji kuwezeshwa ili kuweza kujikwamua ambapo CAMFED inahusika kuwawezesha kupata elimu kutimiza ndoto zao ambapo ufadhili unaofanywa na CAMFED ni kwa watoto walioko mashuleni, waliomaliza kidato cha nne na kutaka kurudia mitihani lakini pia wanaohitaji kufanya mitihani ya QT sambamba na wale wanaotaka kujifunza masuala mbalimbali ya ujasiriamali.

Naye mratibu wa CAMFED Wilaya ya Kilosa na Gairo Zamoyoni Salehe amesema kwa kiasi imejikita katika kumpatia mtoto wa kike elimu na kuwawezesha kufanya miradi mbalimbali kwa kupata mikopo ambayo haina riba ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kwamba lengo la kutoa fursa ya kujikwamua ni kumfanya mtoto wa kike ajione kuwa anaweza na si kuwa tegemezi.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Grace Chogogwe amewataka watoto hao wakike kuthamini ufadhili unaotolewa na CAMFED na kwamba wakati wa ujana ndio wakati wa kuumba maisha yao hivyo ujuzi wataopata wauzingatie na kuutumia vizuri katika maisha yao huku mwalimu wa chuo hicho Ginslar Ngonyani akiwataka kutumia fursa hiyo vizuri kwa kuhakikisha wapatapo mafunzo hayo kuwa na shughuli zao ili kuepuka vishawishi ambavyo hutokana na kukosa shughuli za kufanya ambapo amesema chuo cha maendeleo ya wananchi Ilonga kinatoa mafunzo mbalimbali ikiwemo ufundi uashi, ujenzi, stadi za umeme, ushonaji na nyinginezo na kwamba kinawakaribisha sana chuoni hapo ambapo mwalimu huyo pamoja na wenzake waliwatembeza watoto hao kujionea namna watoto wakike waliopo chuoni hapo wanavyojifunza na kufanya stadi mbalimbali .
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa