Mifumo mipya ya kielektroniki ya usimamizi wa utendaji kazi katika utumishi wa umma (PEPMISnaPIPMIS) imeanzishwa ili kumaliza changamoto za mifumo iliyokuwepo ya kiutumishi kama vile OPRAS lakini pia itawawezesha watumishi kujipima utendaji kazi wao wenyewe pamoja na kupata huduma nyingine za kiutumishi kama vile kuomba uhamisho au kuomba mkopo wenyewe kwa njia ya mtandao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, kutoka Ofisi ya RaisUtumishiBw. Priscus Kiwango wakati akifungua mafunzo Kwa watumishi wa tarafa ya MIkumi wilayani Kilosa yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Cha Ufundi VETA Mikumi
Bw. Priscus ameongeza kuwa lengo la serikali kuanzisha mifumo hii ni kujenga uwezo wa taasisi za Umma kuhusu masuala ya usimamizi wa utendajikazi kwa watumishi na Taasisi za Umma lakini pia mfumo huu utachochea uwajibikaji wa hiari, kuondoa upimaji usiohakisi uhalisia.
Ameongeza kuwa mfumo huo utamwezesha mtumishi kujitathmini utendaji kazi wake Kwa asilimia 70 na kumwezesha kukata rufaa iwapo hatoridhika na alivyotendewa na mkuu wake wa kazi.
Akizungumzia changamoto zaOPRAS na IPCS mkufunzi wa mifumo hiyo Paul Magesa Mashauri amesema kuwa haikuwa na uwezo wa kutofautisha kada zote bila kujali aina au utofauti wa majukumu anayotekeleza mtumishi lakini pia mifumo hiyo kutokidhi hali halisi ya utendaji kazi wa watumishi hali iliyoleta hisa za kupendeleana au kuoneana.
Kwa upande wake Hafisa Utumishi wa Halmashauri ya Kilosa Winfred Mhwagila amewataka watumishi kuwajibika kujaza taarifa sahihi kwenye mfumo na kuwataka watumishi ambao hawajajisajili wajisajili Ili kufikia tarehe 01/01/2024 taarifa Kwa watumishi wote zianze kuwekwa kwenye mfumo huo.
Pia amewataka watumishi walioudhuria mafunzo kuwafundisha namna ya kutumia mfumo wale watumishi walio chini yao ambao hawajahudhuria mafunzo.
Mafunzo hayo Kwa wilaya ya Kilosa yamefanyika katika tarafa za Mikumi, Kilosa na Dumila huku watumishi wasimamizi wa kada zote wameudhuria mafunzo hayo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa