Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg Michael John Gimile amewataka Watumishi wote kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kanuni, Sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali lengo likiwa ni kuwaletea maendeleo Wananchi kama ilivyokusudiwa
Amesema hayo Aprili 27, 2024 wakati wa kikao chake na Watumishi wa Divisheni na vitengo vyote kutoka Makao Makuu ya Halmashauri, kikiwa na lengo la kujitambulisha rasmi na kukumbushana masuala mbalimbali ya kiutumishi ambapo pamoja na mambo mengine amesititiza nidhamu, itifaki ya mawasiliano kazini, pamoja na haki na wajibu wa mtumishi.
Ndg Gwimile amesema kila mtumishi anapaswa kuzingatia Sheria,Taratibu na kanuni zilizowekwa na Serikali na kwamba hiyo itasaidia katika kumuongoza kufanya masuala mbalimbali pindi anapokuwa katika kutimiza majukumu yake,pia amesisitiza kuwa kila mtumishi kwa nafasi yake kusimamia taratibu zilizowekwa na kufanya kazi kwa bidii ili kuwaletea Wananchi maendeleo.
Naye Mkuu wa Divisheni ya Utawala na usimamizi wa Rasilimali watu Ndg Betuely Joseph Ruhega amesema kuwa kutokana na Wimbi la watumishi wanaostaafu Utumishi wa Umma kujikuta katika changamoto mbalimbali za kimaisha Hususan za kiuchumi mara baada ya kustaafu hali inayopelekea kupata maradhi au hata kufa amewaasa watumishi kujiandaa kustaafu mara tu wanapoanza safari yao ya ajira.
Ndg Ruhega amesema kuwa endapo Mtumishi akijiandaa mapema kiuchumi na kijamii suala la kustaafu kwa namna yeyote ile halitamsumbua hivyo amewata watumishi kujifunza kuweka akiba na kuacha tabia ya kutegemea chanzo kimoja cha mapatao kwani hiyo inapelekea watumishi wengi kuishi maisha ya kubahatisha.
Aidha amewataka watumishi kutafuta vyanzo vingine vya mapato tofauti na mshahara ili hata wanapomaliza utumishi wao Serikalini tayari wanakuwa wameshajikita katika jambo Fulani na hii itawaepushia kukurupuka kuingia kwenye biashara wasizokuwa na uzoefu nazo na kupelekea kuanguka kiuchumi na wakati mwingine kuwasababishia msongo wa mawazo au vifo vya mapema
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa