Watumishi wa umma wametakiwa kushiriki ipasavyo katika matukio ya kitaifa yanayotarajiwa kufanyika ndani ya Halmashauri hivi karibuni ikiwemo uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura pamoja na Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi na Ununuzi Grace Nyabanje kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri katika kikao cha robo ya pili cha Watumishi wote wa makao makuu ya Halmashauri kilichofanyika 14 Februari, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri.
Amewataka Watumishi hao kushiriki katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linalotajia kuanza tarehe 01 Machi, 2025 hadi 07 Machi, 2025 lakini pia mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa 18 Aprili, 2025.
Bi. Grace amesisitiza kuwa kila mtumishi kwa nafasi yake anatakiwa kushiriki kuanzia maandalizi hadi utekelezaji wake ili kukamilisha matukio hayo mawili.
Kwa upande wake Mkuuwa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Betuely Ruhega amewataka watumishi kuzingatia kanuni za kiutumishi wa Umma katika utendaji kazi wao wa kila siku.
Amewataka kuwahi kazini lakini pia kuacha utoro wa reja reja kwani kufanya hivyo ni kinyume cha kanuni za utumishi wa Umma.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa