Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa wamepatiwa mafunzo juu ya kutumia Mfumo wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma ,(PSSSF Portal )utakao wawezesha kufuatilia na kukagua kwa ukaribu taarifa za michango kupitia simu janja ili kama kuna changamoto ziweze kutatuliwa kwa wakati kipindi ambacho bado wapo kazini.
Hayo yamebainishwa 16 Mei, 2024 na Mkaguzi Mwandamizi kutoka Ofisi ya PSSSF Kanda ya Mashariki Morogoro Ndg. Edward Clement Kyungu ambapo amesema kuwa wanachama wengi wa PSSSF wamekuwa wazito kufuatilia suala hilo la msingi jambo linalopelekea kupata usumbufu mkubwa pindi wanapofuatilia mafao mbalimbali hivyo amewataka kuwa na utaratibu wa kuhakiki taarifa zao mbalimbali ili kuondoa changamoto zinazoweza kujitokeza pindi watakapohitaji huduma.
Kupitia mfumo huo Mtumishi anaweza kuhuisha taarifa zake muhimu kiganjani mwake na kwamba haitomlazimu kwenda moja kwa moja katika ofisi husika hivyo kuokoa muda na gharama zisizo na ulazima.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa