Watumishi wapya kutoka Idara za Afya ,Elimu msingi na sekondari wametakiwa kujua kuwa wanajukumu la kutumikia jamii pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ili kuleta maendeleo chanya kwa jamii ya Kilosa.
Rai hiyo imetolewa Julai 4, 2023 na Mkugugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg.Kisena Mabuba wakati akizungumza na watumishi hao na kusema kuwa wanapaswa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma sambamba na kufanya shughuli za kuwapatia kipato halali jambo litakalowasaidia kutunza ajira zao.
Kwa upande wake Afisa Utumishi na Utawala Bi. Fauzia Nombo amewataka watumishi hao kuuzingatia wajibu wao kwa kuhakikisha wanafuata sheria kanuni na taratibu za kiutumishi ,huku Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt .Mameritha Basike akisisitiza suala la utunzaji wa siri kwa jamii watakazo zihudumia .
Naye Mkuu wa Divisheni ya elimu Sekondari Joseph Kapere na Mkuu wa Divisheni ya Elimu Msingi bi Zakia Fandey wamewataka watumishi hao kufahamu mifumo mbalimbali iliyotolewa na Serikali kwaajili ya utendaji kazi sambamba na kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa Miradi ya maendeleo ili kuleta tija kwani Serikali imewaamini na kuwategemea.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa