Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Joseph Kakunda amewataka wafanyakazi wa umma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa kuzijua vema kanuni za utumishi kwani kujua kanuni za utumishi kutasaidia watumishi hao kufanya kazi kwa weledi, kuipenda na kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.
Kakunda amesema hayo Agosti 3, 2018 alipotembelea halmashauri hiyo kwa ziara ya siku moja na kuongea na wafanyakazi wa halmashauri hiyo ambapo amewasisitiza watumishi kuhakikisha kila mmoja anayafahamu vizuri majukumu yake na kuwajibika ipasavyo ili kuunga mkono kauli mbiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu.
’’Aidha niwasisitize jambo hili muhimu kuwa licha ya kufahamu kanuni za utumishi kila mmoja wenu anapaswa kuonyesha uwezo wake kwa kazi ambao unapaswa kuwa wa kiwango cha juu ambapo matokeo ya uwezo wa kazi kuwa juu ni kuwa na maendeleo halikadhalika majukumu ya kila mmoja yatakuwa yametekelezwa kwa kiwango cha juu hali itakayopelekea nchi, mkoa, wilaya kuwa na maendeleo’’. Kakunda ameongeza
Sambamba na hayo amewataka watumishi hao kuwa na mahusiano mazuri na familia zao pamoja na viongozi wanaowaongoza pasipo kujali kiongozi aliyeko madarakani kama ni mkubwa au mdogo bali heshima ishike mkondo wake kwani kiongozi aliyeko madaraka ameaminiwa na mamlaka iliyomuweka eneo husika na ana dhamana ya kuongoza eneo hilo, hivyo anapaswa kuheshimiwa hata kama umri wake ni mdogo.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa