Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu kwani kwasasa elimu inatolewa bila malipo, hivyo kila mzazi ahakikishe mtoto anapata fursa ya kupata elimu ambayo itamsaidia katika maisha yake lakini pia kuwalea katika maadili mema kwa kuwarithisha mila na desturi njema ili kuwa taifa lenye sifa njema na maadili mema.
Wito huo umetolewa Januari 30, 2023 na Katibu Mkuu CCM Comrade Daniel G. Chongolo katika ziara yake ya kufatilia utekelezaji wa ilani ya CCM ambapo amewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanapata elimu ambayo inatolewa bila malipo na kwamba mtoto anapopata elimu inamsaidia kupata fursa mbalimbali katika ajira.
Comrade Chongolo amesema kuwa watoto wanapopata elimu ni rahisi kuingia katika sekta mbalimbali ili kujipatia ajira kwani ili kizazi cha sasa kiweze kuwa cha ushindani ni lazima kipate elimu ili kuweza kumudu ushindani wa fursa mbalimbali lakini pia itasaidia kutoa elimu katika familia zao katika masuala mbalimbali ili kujiletea maendeleo yao na familia zao.
Aidha katika ziara yake ametembelea katika shule za sekondari za Maguha na Mikumi na kuwapatia zawadi ya jezi na mipira miwili toka kwa Mheshimiwa Rais wa awamu ya sita kwa shule zote mbili ambapo pia ametaka kukamilishwa kwa miundombinu ya nishati ya umeme ambayo haijakamilika ili nishati ya umeme iweze kupatikana katika shule ya sekondari ya Maguha ambayo ni mpya, ambapo pia amewapongeza wananchi wa Kilosa kwa juhudi wanazofanya katika kujiletea maendeleo kwa kushiriki shughuli za maendeleo.
Pamoja na hayo ametaka wanakilosa kuunga mkono juhudi mbalimbali zilizofanywa na Serikali kwa kutunza miundombinu mbalimbali iliyopo ndani ya wilaya kwa kuhakikisha inatunzwa ili iweze kutumika kwa muda mrefu huku upande wa mashamba yaliyofutwa na Mheshimiwa Rais amesema Waziri wa kilimo atafika wilayani Kilosa ili kusikiliza wakulima ili yaweze kutolewa maamuzi sahihi dhidi ya changamoto za wakulima katika matumizi sahihi ya mashamba hayo.
Kwa upande wa mbunge wa jimbo la Kilosa Mh. Prof Palamagamba Kabudi na Mh. Dennis Londo mbunge wa jimbo la Mikumi wameshkuru juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kiwemo kufutwa kwa mashamba 11 na kugawiwa kwa wananchi sambamba na mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu, afya, uboreshwaji wa miundombinu na miradi mbalimbali ya maendeleo na kwamba wanaamini uwepo wa reli ya kisasa utakuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa wananchi wa Kilosa na nchi kiujumla.
Katika ziara yake ya siku moja Comrade Chongolo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari Maguha, Upanuzi wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi, barabara ya kiwango cha lami Rudewa – Kilosa, Reli ya kisasa ya mwemdo kasi(SGR), shule ya Sekondari Mikumi pamona na kusalimiana na wananchi katika kata za Dumila, Maguha, Mabwerebwere, Ulaya, ,henda na Mikumi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa