Waziri wa Ujenzi Innocenti Bashungwa amemtaka mkandarasi anayejenga madaraja matatu barabara ya Dumila Kilosa kukamilisha Ujenzi huo kabla ya Aprili 22, 2024 Ili kuwaondolea kadhia ya usafiri watumiaji wa barabara hiyo.
Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika February 22, 2024 katika daraja la Mazinyungu alipotembelea wilayani Kilosa kujionea hali ya miundombinu ilivyo baada ya mafuriko yaliyoyakumba baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo na kusababisha uharibifu mkubwa wa barabara na madaraja.
Amesema kuwa tayari serikali imeshamlipa mkandarasi huyo hana budi kukamilisha Ujenzi huo kwa muda waliokubaliana Ili yaanze kutumia,Aidha amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha Kwa ajili ya Ujenzi wa miundombinu zikiwemo Barabara na madaraja.
Ameongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuufungua Mkoa wa Morogoro Kwa kujenga barabara inayoiunganisha mikoa ya Njombe, Lindi, Morogoro na Tanga kupitia wilaya za Kilombero, Kilosa na Kilindi mkoani Tanga Ili kuwawezesha wananchi hususani wa Wilaya ya Kilosa kufanya biashara kupitia barabara hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe Adamu Malima amemshukuru waziri Bashungwa Kwa kuitembelea wilaya ya Kilosa na Mkoa mzima Kwa ujumla Ili kujionea hali ya miundombinu ilivyo.
Naye mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi amuomba waziri kupitia wizara yake kuwekwa Kwa taa za barabarani kuanzia maeneo ya Njia panda ya Ilonga hadi zilipo Ofisi za mkuu wilaya.
Aidha ameiomba wizara kuleta vifaa vya kupunguza mchanga katika mto Mazinyungu Ili kuongeza kina cha mto huo kwani maji ya mto huo yamekuwa yakisababisha mafuriko hasa kipindi cha mvua kubwa kutokana kina cha mto huo kujaa mchanga.
Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka ametoa shukrani zake Kwa serikali Kwa Kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo wilayani humo na kuahidi kuendelea kuisimamia na kuitunza miradi hiyo zikiwemo barabara na madaraja.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa