Waziri wa Nchi Ofisi ya RaisTawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohamed Mchengerwa amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg Michael John Gwimile kuendelea kudhibiti mapato ya Halmashauri ili kuweza kujiendesha bila kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu.
Waziri Mchengerwa ametoa maagizo hayo Mei 20, 2024 alipotembelea kituo cha Afya cha Mikumi Wilayani hapa ikiwa ni ziara yake ya siku 5 Mkoani Morogoro yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa.
Aidha, Mhe. Mchengerwa amemtaka Mkugenzi huyo na timu yake kubuni na kutekeleza Miradi ya Maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani ikiwemo miradi ya Afya na miradi mingine lengo likiwa ni kutoa huduma kwa wananchi.
Sambamba na hilo, Mhe. Mohamed Mngerwa amewaagiza Mganga Mkuu wa Mkoa na Mganga Mkuu wa Wilaya kusimamia vyema vituo vya afya huku akiahidi kuongeza upatikanaji wa dawa na ujenzi wa zahanati ndani ya wilaya ya Kilosa kutokana na uhitaji mkubwa wa huduma ya afya uliopo.
Katika Ziara yake Wilayani kilosa Mhe Mchengerwa ametembelea Daraja la Ruhembe kata ya Ruhembe, Kituo cha Afya Mikumi kata ya Mikumi na Shule ya Sekondari ya Miwa Kata ya Ruhembe.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa