Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa ameonyesha kuridhishwa kwake na ujenzi wa mradi wa reli ya mwendo kasi hususani ujenzi wa handaki la urefu wa kilometa 1 unaoendelea kujengwawilayani Kilosa ambao kwa sasa umefikia takribani asilimia 83 ya ujenzi huo ili handaki hilo kukamilika.
Majaliwa ameonesha kuridhishwa mara baada ya kutembelea ujenzi wa mradi huo Mei 14 mwaka huu na kusema kuwa katika ziara yake ya kukagua mradi huo toka Dare s salaam hadi Morogoro ameridhishwa na utaalam, kasi na kazi ya ujenzi unaoendelea pamoja na hatua iliyofikiwa
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewasihi watanzania waliopata kazi katika kampuni ya Yarp Merkez inayojenga reli hiyo kuongeza nguvu ya ujenzi ili kumaliza ujenzi huo mapema iwezekanavyo.
Akizungumzia reli hiyo namna itakavyofanya kazi amesema mradi huo ni mradi wa kimakakati utakaokuza uchumi wa nchi huku akisema kuwa pamoja na uchumi kupanda lakini pia umetatua changamoto ya ajira kwa watanzania ambapo awali vijana wengi walikuwa wakikaa vijiweni lakini kupitia reli hiyo jumla ya vijana 18000 wamepata ajira
Aidha, Waziri Mkuu amesema reli hiyo itakayokuwa ikiendeshwa kwa umeme haitasimama kufanya kazi kwa sababui ya ukosefu wa nishati ya umeme kwa kuwa reri hiyo itaunganishwa na vyanzo vitatu vya uhakika vya umeme ikiwemo bwawa la mwalimu Nyerere, Kidatu Mtera na umeme wa Kinyerezi unaotokana na gesi.
Amesema endapo vyanzo vyote hivyo umeme wake ukikatika reli itaendelea kufanya kazi kwa kutumia mtambo maalum ambayo itafungwa kwenye reli yenyewe ikiwa na uwezo wa kutunza umeme kwa dakika 45.
Akitoa rai kwa watanzania waliopata ajira kwenye mradi huo Majaliwa amewataka kutumia fursa hiyo kwa kujenga uaminifu na kuepuka dosari za kukosa uaminifu huku akiwataka kupata ujuzi na kuwa wataalam kwa siku za baadae kwa kuhakikisha wanajituma katika sekta walizopo ili baadae waweze kujiajiri ama kuajiri vijana wengine pamoja na kuomba tenda katika miradi mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa