Waziri wa katiba na sheria ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kilosa Mhe. profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa mabadiliko makubwa katika sheria za uchaguzi nchini Tanzania yameongeza wigo wa demokrasia kwa kutoa fursa kwa wananchi kumchagua mgombea ambaye amepita bila kupingwa.
Prof. Kabudi aliyasema hayo baada ya kupiga kura katika kituo cha Manzese kilichopo katika jimbo lake la kilosa mapema Novemba 27,2024 ambapo waziri huyo alisema kuwa ni mara ya kwanza kwa wananchi waliopita bila kupingwa kushiriki katika mchakato wa uchaguzi kwa kupiga kura.
Amesema mabadiliko hayo yana umuhimu mkubwa katilka kuhakikisha kuwa demokrasia nchini inaendelea kukua na kwamba wananchi wanapata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa