Katika kuinua sekta ya afya Wilaya ya Kilosa imeimarisha huduma za afya kwa kuimarisha huduma za uzazi kwa wanawake na kinamama wajawazito kwa kufungua wodi mpya ya wazazi ambayo imeanza kufanya kazi na kutoa huduma kwa kinamama wajawazito na waliojifungua ambayo imeboreshwa na kutegemewa kutoa huduma zote katika jengo moja tofauti na jengo la awali.
MKUU WA KITENGO CHA WODI YA WAZAZI BI SARA ELIAH AKIWA OFISINI KWAKE
Hayo yamebainishwa Januari 22 mwaka huu na Mkuu wa kitengo cha Wodi ya Wazazi katika hospitali ya Wilaya Sarah Eliah ambapo amesema kuwa wodi hiyo imeanza kazi Januari 21 mwaka huu ambapo amesema kuanza kutumika kwa wodi hiyo kumekuwa mkombozi kwa kiasi kikubwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinawakabili kiutendaji kazi, kinamama wajawazito na kinamama waliojifungua kwani jengo la awali lilikuwa dogo, chakavu na lisilotosheleza kihuduma pia baadhi ya miundombinu yake haikuwa bora na kuvuja baadhi ya maeneo tofauti na jengo la sasa ambalo ni kubwa na linatarajiwa kutoa huduma muhimu za kinamama kwa urahisi katika jengo moja.
MMOJA WA WAUGUZI AKIWA KATIKA MAJUKUMU YAKE KATIKA WODI YA WAZAZI
Bi Elia amesema pamoja na jengo kujitosheleza zipo baadhi ya changamoto ikiwemo ufinyu wa vyumba kwa ajili ya kinamama wanaojisubiria kujifungua kuwa vichache na vidogo, miundombinu ya umeme bado haijakaa sawa kuwa na umeme wa kutosheleza kwa jengo zima, miundombinu kwajili ya kubebea wakinamama kabla ya kuwapeleka chumba cha upasuaji kwa ajili ya kujifungua ambapo kwa sasa kinamama wajawazito wanaopaswa kujifungua kwa njia ya upasuaji wanalazimika kutembea kwenda jengo la upasuaji pamoja na nguvu ya maji kuwa ndogo kipindi ambacho hakuna umeme.
Licha ya changamoto hizo ameushukuru uongozi wa Wilaya kwa hatua zilizofikiwa na juhudi zilizoonyeshwa katika kuboresha huduma za afya ambapo pia ameshauri kuongezwa kwa vyumba vingine viwili ili kuweza kukidhi mahitaji ya wateja kwani zipo nyakati ambazo hupokea wakina mama wajawazito wengi takribani 10 hadi 15 kwa siku hivyo kwa hali hiyo itapelekea kuwa na uhaba wa vyumba, aidha amesema upande wa vyoo katika jengo hilo jipya ni vya kutosha hivyo kupelekea kinamama kuwa salama kiafya dhidi ya magonjwa mbalimbali ya maambukizi tofauti na jengo la awali ambalo shimo la choo lilikuwa ni moja.
BAADHI YA KINA MAMA WAJAWAZITO WANAOJISUBIRIA KUJIFUNGUA WAKIWA WODINI
Kwa upande wa kinamama wajawazito na wazazi waliolazwa katika wodi hiyo kwa nyakati tofauti wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Wizara ya Afya kwa ajili ya wodi hiyo kwani mazingira ni mazuri na huduma ni nzuri ambazo wameanza kuzipata lakini pia lina nafasi ya kutosha lakini pia kwasasa usumbufu haupo uliokuwa ukitokana na ndugu waliokuwa wakiingia wodini na kusababisha kelele na usumbufu kwa wauguzi kwani kwa sasa ndugu wote huishia nje ya wodi lakini pia wamesema awali wajawazito na waliojifungua kwa njia ya kawaida walikuwa wanakaa eneo moja lakini kwa sasa hali tofauti ambapo wanaojisubiria wana eneo lao halikadhalika waliojifungua pia wana eneo lao.
BAADHI YA KINAMAMA WALIOJIFUNGUA WAKIWA NA WATOTO WAO KATIKA WODI YA WAZAZI
Kwa upande wa kinamama wajawazito na wazazi waliolazwa katika wodi hiyo kwa nyakati tofauti wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Wizara ya Afya kwa ajili ya wodi hiyo kwani mazingira ni mazuri na huduma ni nzuri ambazo wameanza kuzipata lakini pia lina nafasi ya kutosha lakini pia kwasasa usumbufu haupo uliokuwa ukitokana na ndugu waliokuwa wakiingia wodini na kusababisha kelele na usumbufu kwa wauguzi kwani kwa sasa ndugu wote huishia nje ya wodi lakini pia wamesema awali wajawazito na waliojifungua kwa njia ya kawaida walikuwa wanakaa eneo moja lakini kwa sasa hali tofauti ambapo wanaojisubiria wana eneo lao halikadhalika waliojifungua pia wana eneo lao.
JENGO JIPYA LA WODI YA WAZAZI KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KILOSA
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa