Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka amesema kukamilika kwa shule mpya ya sekondari ya Ruhembe kutapunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa wanafunzi ambapo kwa sasa inawalazimu kutembea kwa zaidi ya kilometa 25 kufuata shule kutokana na kata hiyo kutokuwa na shule ya sekondari.
Mhe. Shaka amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo ambapo moja ya miradi aliotembelea ni mradi wa ujenzi shule ya sekondari Ruhembe unaogharimu zaidi ya shilingi milioni 520.
Sambamba na hayo Shaka amesema kuwa wazazi na walezi wa eneo hilo baada ya kuona adha wanayoipata watoto wao waliamua kujenga vyumba viwili vya madarasa jambo ambalo limemsukuma Mhe Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kuunga mkono wananchi hao kwa kutoa kiasi hicho cha fedha ili kujenga Shule ya Sekondari.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya kilosa Shabani Mdoe amesema chama kitaendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya chama cha Mapinduzi ili ikamilike kwa wakati na Wananchi wapate huduma stahiki na kwa wakati uliopangwa.
Shule hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi novemba 30, 2023.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa