Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kilosa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Amer Mbaraka , imefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa pamoja na Taasisi zilizopo ndani ya Wilaya kwa lengo la kuona utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha miezi sita, Januari –Juni 2023.
Miradi iliyotembelewa ni Pamoja na ujenzi wa barabara ya kilometa 16 kutoka Mvumi mpaka Makwambe,Ujenzi wa vyumba 6 vya madarasa katika shule ya Sekondari Mkundi iliyopo kata ya Dumila,Mradi wa jengo pacha la Mama na Mtoto na Maabara katika kituo cha Afya Magubike.
Sambamba na hayo Kamati hiyo ya Siasa imetembelea Mradi wa REA kata ya Mabula, Mradi wa REA kata ya Tindiga ,Ujenzi wa vyumba 8 vya Madarasa Shule ya Sekondari Kitange II kata ya Mtumbatu,Mradi wa maji kata ya Kidodi, Mradi wa maji pamoja na Soko lililoungua kata ya Ruaha,Mradi wa Daraja kata ya Ruhembe,na Mradi wa Maji kata ya Malolo
Akihitimisha Ziara hiyo Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya amesema kuwa Miradi yenye changamoto ifanyiwe kazi ili ikamilike kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa ili Wananchi wapate huduma stahiki.
Aidha Kamati imeipongeza Serikali chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi mingi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa ili kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa