Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Mizengo Peter Pinda amesema kuwa amefurahishwa na ujenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kinachomilikiwa kwa asilimia 100 na Serikili.
Mh Mizengo Pinda amesema hayo agosti 2,2023 wakati wa ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho cha Sukari Mkulazi kilichopo Wilayani Kilosa kwa lengo la kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho ambapo ameonesha kuridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Aidha Mh Pinda amesema uchumi wa Wananchi utaongezeka kwani Serikali imeanza kuwekeza na kushirikisha Vijana na Wanawake kwenye kilimo hususan cha miwa ili kuweza kuzalisha zao hilo kwa wingi hivyo kupata uzalishaji wa sukari ya kutosha.
Sambamba na hayo Mh Pinda amepongeza juhudi za Mh Rais Dokta Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa ni jambo la kujivunia kwa Serikali kuwa kuwa na uwekezaji mkubwa wa viwanda vya Sukari nchini kwani mbali na kuzalisha Sukari lakini pia kutakuwepo na fursa ya ajira kwa wazawa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Adam Kighoma Malima amesema kuwa ukamilishaji wa kiwanda hicho utasaidia nchi katika mahitaji ya Sukari tani 550,000 hadi 600,000 kwani Morogoro pekee itakuwa inatoa tani 430,000 ndani ya mfumo.
Aidha amepongeza uongozi wa kiwanda hicho na kusema kuwa amefurahishwa na mpango mkakati wa Kiwanda hicho wa kushirikiana na Wakulima wa Miwa ili kuzalisha malighafi za kutosha za kulisha kiwanda sambamba na kupata ujira wao.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa