Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amewataka Viongozi wa nafasi zote Wilayani Kilosa kuzifanyia kazi changamoto na kero zinazowakabili wananchi kwani wameaminiwa na kupewa dhamana ya kuongoza na kuleta maendeleo kwa Wananchi.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema hayo Julai 27, 2023 wakati wa Ziara yake ya kutembelea kata ya Mamboya kwaajili ya kusikiliza kero, ushauri na mipango ya kuimarisha shughuli za maendeleo ya kata na Wilaya nzima kwa ujumla.
Mh Shaka amesema kuwa kila kiongozi anapaswa kutenda haki kwani kila aliyepo madarakani ni ishara ya kwamba ameaminiwa na Mh Raisi Dokta Samia Suluhu Hassan hivyo ni vema kutumia nafasi hiyo kwa kufanya yaliyo sahihi ili kuwaletea maendeleo wananchi na kwamba yeye kama Kiranja Mkuu ataendelea kupokea changamoto zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi kwa kushirikiana na viongozi wengine.
Amesema lengo la ziara hiyo ya awamu ya kwanza ya kata kwa kata ni kusikiliza kero, kujifunza na pia kufanya maamuzi magumu pale inapohitajika kufanya hivyo bila kuangalia nafasi ya mtu iwe kwa mwananchi wa kawaida au kiongozi ilimradi tu akijiridhisha kama kuna makosa yamefanyika.
Kwa upande mwingine Afisa Mipango miji bw.Hilal Hamisi amezungumza juu ya mgogoro wa mipaka kati ya Mamboya na Berega uliolalamikiwa na Wananchi wa kata ya Mamboya na kusema kuwa suala hilo wanalifahamu na kuahidi kulifanyia kazi mpaka ifikapo septemba mwaka huu.
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa