Imebainika kuwa shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania (TFSG) kwa kushirikiana na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kupitia mradi wa mkaa endelevu umeonekana kuwa na tija hasa katika kukuza ushirikiano na mahusiano yanayolenga kuboresha uwezo wa wanachama wake wa kujihusisha kwa ukamilifu na usimamizi na uhifadhi wa misitu, kutetea kuongezeka kwa umiliki na matumizi bora ya ardhi na misitu kwa ajili ya kuboresha maisha ya jamii.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Adam Mgoyi wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Wazi ya Shughuli za Mradi wa Mkaa Endelevu na miradi ya maendeleo katika kijiji cha Ulaya Mbuyuni wilayani Kilosa ambapo amesema kuwa Mungu ametutunukia bahati ambayo tunapaswa kuitunza na kuitumia vizuri huku tukizingatia kanuni na sheria za matumizi bora ya ardhi kwani hakuna jambo zuri linaloweza kufanyika bila mpangilio.
Mgoyi amesema ni vema sheria na matumizi bora ya ardhi yakazingatiwa na kutumika inavyopaswa, hivyo kila kiongozi afanye majukumu yake kwa kusimamia misitu isikatwe hovyo bali kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu kutoka TFSG na MJUMITA kwani kwa kufanya hivyo migogoro haitakuwepo, ambapo katika maonyesho hayo Mkuu wa Wilaya ametembelea msitu wa hifadhi ya kijiji cha Ulaya Mbuyuni na eneo lililotengwa kwa ajili ya uzalishaji mkaa endelevu na kuzindua kisima cha maji.
Sambamba na hayo Meneja Mradi wa Mkaa Endelevu Bw.Charles Leonard amesema mradi wa mkaa endelevu kwa sasa wilayani Kilosa unafanya kazi katika vijiji ishirini vya Kisanga, Msimba, Ihombwe, Kitunduweta, Mhenda, Kigunga, Ulaya Mbuyuni, Ulaya Kibaoni, Dodoma Isanga, Nyali,Unone, Rudewa Gongoni, Mvumi, Makwambe, Gongwe, Kisongwe, Chabima, Mbamba, Mfuluni na Zombo.........
Halmashauri ya Wilaya Kilosa
Sanduku la posta: S.L.P 65 Kilosa
Simu: 023 2623093
Simu: 0737847880
Barua Pepe: ded@kilosadc.go.tz
Hatimiliki imehifadhiwa ©2017 Halmashauri ya Wilaya Kilosa